SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI - News Today in World

SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI

SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI
link : SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI

news-today.world |
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe na vitendo vya wizi, ufisadi kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume za kuwachunguza bali itawashughulikia hapo hapo.

Amesema Serikali haikotayari kuwavumilia watumishi wanaojihusisha na wizi, ubadhilifu, rushwa na uzembe, hivyo ni vema viongozi waliopewa dhamana wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Januari 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Musoma mkoani Mara akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani hapa.

“Fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo zinalenga kutatua kero za wananchi na si kuwanufaisha wachache wenye tamaa. Kama ni za ujenzi wa zahanati ijengwe na atakayezitafuna Serikali haitosita kumchukulia hatua.”

Waziri Mkuu asiwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa mujibu wa sharia kwa sababu vitendo vya wizi, uzembe vinachangia kupunguza kasi ya kuwaletea maendelea maendeleo Watanzania.

Alisema lengo ni kuhakikisha azma ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi hususan ni wale wa hali ya chini inatimia, hivyo aliwaagiza viongozi wa halmashauri wakiwemo Madiwani kusimamia vizuri miradi ya maendeleo.

Pia Waziri Mkuu aliwataka wakuu wa idara na watendaji wengine wa halmashauri kuacha tabia ya kukaa ofisini na dabala yake waende vijijini kwa ajili ya kuwafuata wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Waziri Mkuu alisema watendaji hao wanatakiwa waachane na tabia ya kuwasubiri wananchi wawapelekee malalamiko yao kwa sababu baadhi yao hawana uwezo wa kufika katika ofisi zao.


That's an article SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI

Fine for article SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article SERIKALI KUTOSUBIRI KUWAUNDIA TUME MAFISADI NA WEZI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/01/serikali-kutosubiri-kuwaundia-tume.html

Subscribe to receive free email updates: