WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI - News Today in World

WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI
link : WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

newstoday-ok.blogspot.com ~
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akishiriki dua ya kumuombea marehemu ya aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, akisaini kitabu cha maombolezo, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro, wakati akiwasili kwenye msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, (katikati) ni Katibu Mkuu Ikulu Alphayo Kidata, Julai 7, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitoa pole kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
 ********************
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi kuuaga mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Bw. Hassan Shebuge.

Marehemu Bw. Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7,2017) nyumbani kwake Mbagala- Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Julai 8, 2017), katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.

Bw. Shebuge amefariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata na shinikizo la damu.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali.

Amesema enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na kutoa  mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa ufanisi. 

“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.”

Awali, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Bw. Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.

Alisema marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani Tanga.

Bw. Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha sita. 

Alisema mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.


That's an article WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

Fine for article WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article WAZIRI MKUU ASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/waziri-mkuu-ashiriki-kuaga-mwili-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :