SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART
SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post
Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.
Title : SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART
link : SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART
You are now reading the article SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/05/serikali-yakusudia-kutafuta-mbia.html
Title : SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART
link : SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART
news-today.world |
SERIKALI imesema inakusudia kuongeza mtoa huduma mwingine katika uendeshaji wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) ambayeataingiza mabasi yake na kutathmini ufanisi wa mbia wa sasa ili kuimarisha huduma ya usafiri Jijini Dar es salaam .
Amesema iwapo itabainika kwamba mwendeshaji wa sasa ana matatizo yaliyokithiri, Serikali haitasita kumuondoa na kumpa mwendeshaji mwingine kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa uhakika.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 10, 2018) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Bw.Maulid Mtulya katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.
Katika swali lake Bw. Mtulia alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya uboreshaji wa wa mradi wa UDART unaotoa huduma ya usafirishaji wa abiria Jijini Dar Es Salaam ili kuweza kuwaondolea wananchi changamoto ya usafiri.
“Tunatafuta mbia mwingine aweze kuingiza mabasi yake kwenye mradi huu ili aweze kuongeza ushindani na nasi tupate kupata huduma bora kwa maana ya ushindani utaongeza huduma bora zaidi,” amesisitiza.
Waziri Mkuu ameongeza kuwawako wawekezaji wa ndani na nje ukiwemo Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar Es Salaam (UWADAR) ambao wameonyesha nia na uwezo wa kutoa huduma hiyo na kuufanya mradi huo kutoa huduma kwa ubora unaotakiwa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Mheshimiwa Spika Kupitia Bunge lako tukufu, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Maafisa Afya wasimamie zoezi la usafi na kuboresha miundombinu yote na utawapima kupitia zoezi hili,” amesema.
Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kutatua tatizo la usafi wa mazingira pamoja na miundombinu hususani katika masoko hali ya kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakusanya fedha nyingi bila kuboresha maeneo na kukithiri kwa uchafu.
Waziri Mkuu amesema suala la usafi limekuwa likifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi baada ya kuasisiwa na Rais Dkt. John Magufuli, hivyo ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji hao wahakikishe maeneo yao yanakuwa safi na miundombinu inayoweza kutumika wakati wote.
That's an article SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART
Fine for article SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.
You are now reading the article SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/05/serikali-yakusudia-kutafuta-mbia.html