MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA - News Today in World

MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA

MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA
link : MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA

news-today.world |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Aprili 1, 2018 akiwa njiani kuelekea Geita ambako leo, Aprili 2, 2018 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwasha Mwenge wa Uhuru. Kiulia ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 *******************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa mkoa wa Mwanza kuendelea na usaji wa wanunuzi wa zao la pamba na wawape fursa ya kuchagua maeneo wanayotaka kununua pamba.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumapili, Aprili 02, 2018) alipozungumza na viongozi mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa njiani kuelekea mkoani Geita.

Waziri Mkuu leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwasha mwenge wa Uhuru zitakazofanyika mkoani Geita. Kauli mbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’

Waziri Mkuu alisema wakati viongozi hao wakiendelea na usajili wa wanunuzi wa pamba ni vema wakawapa nafasi ya kuchagua maeneo watakayohitaji kukunua kwa sababu yanaweza kurahisishia usafirishaji.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwasisitiza viongozi hao kuendelea kusimamia na kufuatilia maendeleo ya zao hilo kwa umakini zaidi ili kuweza kubaini changamoto zitakazojitokea na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.

Alisema kutokana na mwenendo wa hali ya hewa mwaka huu wakulima wa zao la pamba wanatarajiwa kuvuna pamba nyingi, hivyo ni vema ukatengenezwa utaratibu utakaomrahisishia mkulima kutoa mazao shambani na kufikisha mnadani.

Waziri Mkuu alisema utaratibu huo wa kutoa mazao shambani na kupelekwa mnadani kwa wakati ni muhimu kwa sababu utasaidia katika kulinda pamba ili isipoteze ubora wake.

Zao la pamba ni miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali imeamua kuyapa kipaumbe kwa kuyafuatilia kuazia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, pembejeo pamoja na uuzaji. Mengine ni korosho, chai, kahawa na tumbaku.


That's an article MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA

Fine for article MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article MWANZA ENDELEENI KUSAJILI WANUNUZI WA PAMBA-MAJALIWA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/04/mwanza-endeleeni-kusajili-wanunuzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates: