WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA - News Today in World

WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA
link : WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

news-today.world |
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.



Pia amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na utulivu nchini.



Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.



Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ili vijana waweze kupata maendeleo lazima wafanye kazi kwa bidii.



Pia Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani washirikiane na Serikali katika kuimarisha ulinzi na usalama.



Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ukarabati wa kituo cha afya cha Kata ya Mbekenyera na kuwaeleza wananchi dhamira ya Serikali ya kuwahudumia.



Amesema Serikali imetoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia, maabara, wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha upasuaji.


 “Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”


Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

Pia, Waziri Mkuu amekabidhi gari la kubeba wagonjwa katika kituo hicho. Gari hilo limetolewa na Rais Dkt. John Magufuli ili kuimarisha huduma za afya kituoni hapo.


That's an article WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

Fine for article WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article WAZIRI AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/03/waziri-awataka-vijana-wafanye-kazi-kwa.html

Subscribe to receive free email updates: