TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA - News Today in World

TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA

TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA
link : TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA

news-today.world |
Na Anastazia Anyimike, Dodoma
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kanda ya Kati, imekamata magari 15 yakiwemo ya abiria kutokana na kukutwa na bima feki huku wananchi wakitakiwa kuhakiki bima hizo kabla ya kuondoka kwenye ofisi walizonunulia.

Akizungumza jana Meneja wa TIRA kanda ya Kati, Stella Rutaguza alisema katika operesheni iliyofanyika kwa siku tatu mkoani hapa kuanzia Febbruari 26 mwaka huu, imefanya kukamatwa kwa mahari 14 zikiwamo daladala na costa inayofanya asafari zake kati ya Dodoma na Morogoro na magari binafsi.

Alisema katika msako huo  ambao alisema ni endelevu ulihusisha ukaguzi wa magari 586, umewezesha kukamata bajaj tano na pikipiki mbili na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye amehusika kuuuza bima feki.

" Operesheni hii ni endelevu, tunataka kukomesha hali hii ambayo ni hatari kwa watumiaji wa vyombo vya moto na pia uhalifu ambao unalikoseshea taifa mapato," alisema.

Alisema katika operesheni hiyo wamebaini kuwa kuna wale ambao wananunua bima feki wakiwa wanajua ambao wamekuwa wakiuziwa kati ya Sh 5,000 hadi 10,000 kwa stika ya bima yenye thamani kuanzia laki tatu na kuendelea.

" Pia wapo ambao wanauziwa stika za bima feki wakiwa hawajui, na wanauziwa kwa thamani ya fedha ambazo serikali imeweka kulingana na aina ya bima na aina ya chombo cha usafiri," alisema.

Rutaguza amewataka wananchi kuhakikisha wanakagua na kuthibitisha kama bima waliyokata kuwa ni halali wakiwa kwenye ofisi walizokata na kuondokana na tabia ya kulipia bima ka wanaouza bima ambao wanazunguka nazo mtaani.

" Kuna watu wawili tuliwakamata wanasema hawajui waliowauzia bima walikutana na watu hao wakiwa gereji, watu hao bado tunawashikilia kwa sababu haiwezekani stika ya bima amya ni nyaraka muhimu ikauzwa mikononi na wewe ukanunua," alisema


That's an article TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA

Fine for article TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article TIRA KANDA YA KATI YAKAMATA BIMA FEKI KATIKA VYOMBO VYA MOTO DODOMA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/03/tira-kanda-ya-kati-yakamata-bima-feki.html

Subscribe to receive free email updates: