SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018 - News Today in World

SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018

SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018 - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018
link : SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018

news-today.world |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) watashirikiana kwa pamoja kuandaa Maonesho ya Kilimo NaneNane Kitaifa  yatakayofanyika Mkoa wa Simiyu Mwaka 2018.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka amesema kuwa Mkoa utatoa dira ya kuyafanya Maonesho ya Kilimo NaneNane yawe ni Maonesho ya Kilimo Biashara ili Watanzania wapate fursa ya kuona teknolojia mbalimbali kwenye eneo la kilimo, mifugo na uvuvi.
 
“Matarajio yetu kama mkoa kwa kushirikiana na TanTrade ni kuona kwamba tunaingiza Maonesho ya Kilimo NaneNane kuwa tukio ambalo litawakaribisha watu wenye teknolojia mbalimbali Kitaifa na Kimataifa kwenye kuwezesha mageuzi ya kilimo,uvuvi na ufugaji wa nchi kwa kuonesha ni kwa namna gani wanaweza kumfikia mkulima, mvuvi na mfugaji mdogomdogo kwenye teknolojia ya kisasa ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili Maonesho ya Kilimo NaneNane yawekwe kwenye ramani ya dunia” alieleza Mtaka

Aliendelea kwa kuziomba Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali kuyatumia Maonesho haya kuyatangaza kwa kukaribisha makampuni yenye teknolojia kuja kuonesha mkoani Simiyu. 

Mtaka alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwa makundi yote kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika eneo litakalofanyika Maonesho ya Kilimo Biashara ili uwekezaji huo uendane na viwango vya Kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka ameeleza kuwa TanTrade ni taasisi pekee iliyopewa jukumu la kusimamia masuala ya Maonesho ndani na nje ya nchi kisheria.

Hivyo,Rutageruka amesema kutokana na uzoefu wa uandaaji wa Maonesho mbalimbali,  kwa mwaka 2018 Maonesho ya Kilimo Biashara yatakuwa ni Maonesho bora kwasababu watawaandaa washiriki wote Kisekta,  kuweka miundo mbinu ya kisasa na kuyafanya Maonesho haya kuwa ya Kimataifa.

“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ina kiu ya kuona Maonesho ya Kilimo Biashara  yanakuwa ya kisasa  kama ilivyo Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambayo kwa Afrika Mashariki ndio Maonesho yanayoongoza kwa ubora na Maonesho haya ya Kilimo tutayafikisha huko” aliongeza Bw Rutageruka


That's an article SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018

Fine for article SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018 This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article SIMIYU NA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA NANE NANE KWA PAMOJA 2018 With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/03/simiyu-na-tantrade-kuandaa-maonesho-ya.html

Subscribe to receive free email updates: