IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA
IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post
Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.
Title : IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA
link : IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA
You are now reading the article IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/03/igp-sirro-atuma-salamu-za-pasaka.html
Title : IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA
link : IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA
news-today.world |
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro anawashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini. Kiujumla hali ya usalama hapa nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa na jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.
Tunapoelekea kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.
Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya utulivu.
Wazazi wanatakiwa kuwaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu, pia wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.
Vilevile Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia Sheria za Usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Nawatakia Pasaka njema.
Imetolewa na:
Simon Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
That's an article IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA
Fine for article IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.
You are now reading the article IGP SIRRO ATUMA SALAMU ZA PASAKA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/03/igp-sirro-atuma-salamu-za-pasaka.html