WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI - News Today in World

WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI

WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI
link : WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI

news-today.world | Na. Mwandishi Maalum.
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameanza kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi kutoweza kueeneza magonjwa kwa binadamu.

Mpango huo utatoa mwongozo wa namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira kushirikiana katika kuvichukua vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa kuvisafirisha na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, leo tarehe 28 Februari,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu alibainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko hivyo imeamua kuandaa mpango huo ili kuboresha uratibu.

Naye mratibu wa Mkutano huo anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo, alibainisha mpango huo ambao utatoa mwongozo wa sekta za Afya kushirikiana utasaidia kupunguza maabukizi ya vimelea hivyo kwa wanyama na binadamu.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini, ikiwemo wataalamu wanaounda Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, ambao unawajumuisha wataalamu wa kutoka katika sekta zote za afya katika masuala ya maabara.

Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja kwa kushirikiana na Shirika la Maabra SANDIA na DTRA wameandaa mkutano wataalam hao.


That's an article WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI

Fine for article WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/02/wataalam-wa-afya-moja-kuandaa-mpango.html

Subscribe to receive free email updates: