SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI - News Today in World

SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI
link : SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

news-today.world |
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (Kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo ya Viongozi wa Benki wakati wa Mkutano wa majadiliano ya kujiunga katika mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa Mapato katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi wa Benki wakimsikiliza kwa Makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipokua akitoa agizo la kuzipokonya Leseni Benki zote zitakazoshindwa kujiunga na mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa Mapato ifikapo Januari 31, 2018, katika ukunbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa City Bank wakijieleza kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu sababu za kutojiunga na mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa Mapato katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia ) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere wakisikiliza kwa makini hoja za Benki za kuchelewa  kujiunga katika mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa Mapato ikiwemo gharama, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu hatua alizozichukua baada ya Benki kuvunja sheria kwa kutojiunga katika mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa Mapato wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Viongozi wa Benki nchini.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
*************
Benki zote nchini Tanzania na Kampuni za Mawasiliano zinatakiwa kuwa zimejiunga na mfumo wa wa Kielektroniki wa kukusanya mapato kupitia kituo cha Data kilichopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam ifikapo Januari 31, 2018 kinyume na hapo Serikali itanyang’anya Leseni za uendeshaji wa shughuli zao hapa nchini.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Benki Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mwaka 2017 zilitungwa Kanuni za Sheria za utawala wa Kodi ambao ulizitaka Benki na Kampuni za Simu kuwa zimejiunga na Mfumo wa kielektroniki wa kukusanya kodi kati ya Juni, 2017 hadi Desemba 31, 2017 na mpaka sasa ni Benki 27 tu ambazo zimetekeleza hatua hiyo ya Kisheria.

‘Nimekutana na Benki takribani 20 ili kuwasikiliza ni kwanini hawajatekeleza matakwa ya sheria na katika mjadala huo nimebaini sababu kadhaa zilizosababisha baadhi ya Benki kuchelewa kuchukua maamuzi, miongoni mwa sababu hizo ni hofu kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo inaweza kuona miamala na hivyo kuweza kusababisha wizi wa kimtandao” alieleza Dkt. Mpango.

Sababu nyingine ni pamoja na Matakwa hayo kuja ghafla hivyo kuhitaji fedha za dharula na Benki kubwa kama City Bank kuwa na mtandao mkubwa Kimataifa wa nchi takribani 100 hivyo kuwalazimu kuwasiliana na Makao Makuu ya Benki hiyo kabla ya kufanya Maamuzi.

Hata hivyo kwa kuwa tayari wamevunja sheria iliyowataka kutekeleza agizo la Serikali kufikia Desemba 31, 2017, Waziri Mpango amemuagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Charles Kichere kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo faini katika kipindi walichoshindwa kutekeleza sheria.

Dkt. Mpango amezipongeza Benki zilizotekeleza Sheria ndani ya muda uliowekwa kuwa ni pamoja na Exim Bank, Benki ya NMB, Benki ya Posta, Amana Benki, CRDB, China Comnercial Bank, Stanbic na Akiba Commecial Bank na nyingine.
Benki ambazo zipo katika hatua nzuri ni pamoja na I&M, DCB, DTB, Mkombozi Bank, Maendeleo Bank wakati Benki ambazo hazijapiga hatua kuwa ni pamoja na Bank of Africa, Yetu Microfinance Bank, Barclays na Mwanga  Rural community Bank.

Kwa upande wa Mikopo Chechefu katika Benki, Waziri Mpango ameeleza kuwa  hali haikuwa nzuri kwa mwaka 2017 kwa kuwa Mikopo Chechefu ilifikia asilimia 12 ya mikopo yote ya Sekta ya Benki ambapo kwa sasa Wadau wa Benki wameona kuna hatua nzuri katika eneo hilo hivyo kufanya Sekta hiyo kuimarika.
Ameeleza kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iko imara na Sekta ya Benki kwa sasa ina ukwasi wa kutosha na si kweli kama mikopo chechefu inaiangusha sekta hiyo.

Amezitaka Benki  nchini kuwa na mfumo mzuri unaofuata taratibu za mikopo ili kutatua tatizo hilo kwa kukopesha watu wenye vigezo na pia Mahakama imetakiwa kuheshimu dhamana za awali zilizowekwa na wakopaji kwa kuwa kuna wanaokubaliwa dhamana zao na baadaye Mahakama inasema dhamana hizo hazipo halali jambo linaloongeza uwepo wa mikopo hiyo chechefu.


That's an article SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Fine for article SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article SERIKALI KUZIPOKONYA LESENI BENKI AMBAZO HAZITAJIUNGA NA MFUMO WA KIELEKTRONIKI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2018/01/serikali-kuzipokonya-leseni-benki.html

Subscribe to receive free email updates: