TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU
TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post
Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.
Title : TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU
link : TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU
You are now reading the article TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/12/tanesco-yahimiza-matumizi-bora-na.html
Title : TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU
link : TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU
news-today.world |
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MATUMIZI bora ya bonde la Mto Pangani, ndio njia pekee itakayosaidia kutunza vyanzo vya maji ambayo hutumika kuzalisha umeme kwenye vituo vya Pangani Hydro Systems, Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S Mahenda amewaambia wahariri wa vyombo vya habari wanaotembelea bwawa la Nyumba ya Mungu lililoko mpakani mwa wilaya ya Mwanga na Simanjiro.
“Tanesco kama wadau wakubwa wa Mto huu, tumeona Mto umeingia mchanga na mchanga huo unatakiwa kuondolewa ili kuweza kuzalisha maji mengi zaidi kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu na maji hayo yaweze kupatikana kwenye vituo na hatimaye kuzalisha umeme kama ambavyo inatakiwa.” Alisema Mhandisi Mahenda.
Pangani Hydro Systems ni mkusanyiko wa vituo vitatu vya kufua umeme vinavyofuatana ambavyo vimejengwa sehemu tofauti tofauti katika Mto Pangani.
Vituo hivyo ni pamoja na Nyumba ya Mungu, kituo cha Hale na kituo cha New Pangani Falls na vyote kwa ujumla wake huzalisha umeme wa Megawati 97 ambazo huingizwa kwenye Gridi ya Taifa, alisema Mhandisi Mahenda.
Kituo cha Nyumba ya Mungu, kilizinduliwa mwaka 1964 na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, na kina mashine mbili za kufua umeme zilizofungwa tangu mwaka huo na kila moja inao uwezo wa kuzalisha Megawati 4 za Umeme na kufanya jumla ya Megawati 8
Hata hivyo changamoto kubwa inayokikabili kituo hicho na vituo vingine ambavyo vyote huendeshwa kwa kutumia nguvu za maji, ni mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la shughuli za kibinadamu kandokando ya Mto huo pamoja na kwenye bwawa lenyewe na hivyo kupelekea upungufu wa mara kwa mara wa maji ya kutosha kuendesha mitambo.
“Tunashirikiana na wenzetu wanaosimamia bonde la Mto Pangani, kwa kufanya doria za mara kwa mara ili kuwaelimisha wananchi matumizi bora na endelevu ya maji ya Mto huo ili kuleta manufaa kwa pande zote, amesema Mhandisi Mahenda.
Mhandisi Mahenda S. Mahenda(kulia), akifafanua mambo mbalimbali kwa wahariri kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu Desemba 19, 2017
That's an article TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU
Fine for article TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.
You are now reading the article TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/12/tanesco-yahimiza-matumizi-bora-na.html