NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA - News Today in World

NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA

NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA
link : NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA

news-today.world |
 Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson akikabidhi vifaa vya ujenzi kwaajili ya shule ya Sekondari ya Bujela iliyopo Wilayani Rungwe mkoani Mbeya ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa. 
 Wanafunzi wa Bujela  na walimu wao wakiwa katika picha na Naibu Spika.
 Naibu Spika Dk. Tulia Ackson akikabidhi mabati kwaajili ya ujenzi wa Kanisa.
 Dk Tulia akiwashukuru waumini wa Kanisa baada ya kukabidhi msaada wa Mabati.
Naibu Spika Dr Tulia Ackson amefanya ziara katika baadhi ya maeneo Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya ikiwa ni kutekeleza baadhi ya ahadi alizowahi kuzitoa katika kusaidia maendeleo, kwanza alianza kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni tano katika shule ya sekondari Bujela

Akiwa katika shule ya Bujela Dr Tulia alisema “Ndugu zangu niwasihi jambo moja ambalo hata Rais Magufuli husisitiza, tusiingize siasa kwenye mambo ya maendeleo kwasababu  bila hivyo hatutapiga hatua, leo kama TULIA TRUST tuliahidi vifaa vyenye thamani ya Milioni tano na tayari tumetekeleza kwa kuja navyo vikiwemo bati, mbao, mchanga, saruji, chokaa, rangi, vioo, nondo."

“Tunafanya haya yote kwa ajili ya kuhakikisha tunawatengenezea watoto wetu mazingira mazuri ya kujisomea na baadae watuletee maendeleo sisi wazazi wao hivyo niwaombe viongozi wote tushikamane”  alisema Dr Tulia

Safari ikaendelea hadi katika Kanisa la Bujela ambalo liliharibiwa kwa upepo uliosababishwa na mvua huko pia  Dr Tulia alichangia jumla ya mabati 100 Kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa kanisa hilo ambalo tayari ujenzi wake ulianza kwa jitihada za waumini wenyewe kuchangishana kiasi cha fedha.

Dr Tulia aliwahimiza waumini pamoja na viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa la Tanzania amani pamoja na kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kuiongoza nchi salama.


That's an article NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA

Fine for article NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article NAIBU SPIKA TULIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANA BUJELA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/12/naibu-spika-tulia-atimiza-ahadi-yake.html

Subscribe to receive free email updates: