KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO - News Today in World

KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO

KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO
link : KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO

news-today.world |
Mkuu wa Wilaya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama wakiwa wamewashikilia watuhumiwa watano ambao walikutwa na Ng'ombe 93 wakiwa katika Kijiji cha Bukiriro, Kata ya Gwanumpu Tarafa ya Kasanda Wilayani humo wakitokea nchini Burundi.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
KAMATI ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya kakonko ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kanali Hosea Ndagala wamekamata Ng'ombe 93 na raia wanne kutoka Nchi ya Burundi walioingizwa Nchini kinyume cha sheria na wachungaji kutoka Nchini humo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana baada ya oparesheni ya kufukuza mifugu kutoka Nje ya Nchi iliyoingizwa kinyume na utaratibu Mkuu huyo alisema Ng'ombe hizo zilikamatwa katika Kijiji cha Bukiriro kata ya Gwanumpu ambapo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walikuwa wamewahifadhi.

Aidha Ndagala aliwataja wanaoshikiliwa na jeshi la polisi ni Ntirampeba gerald, Ndoayo Yusto, Myosaba Joris na Ndebe Lema wote wakiwa ni raia wa Burundi. Ng'ombe hao waliokamatwa walikuwa wamewekeshwa kwa Bw. Gozbati Moses ng'ombe 27 na Bw. Kaitila Mgiligiji ng'ombe 66 wakazi wa kijiji cha Bukiriro, kata ya Gwanumpu Tarafa ya Kasanda Wilayani humo.

"Niwaombe viongozi Wote hususani wa vijiji vya mpakani kuwajibika na kuhakikisha kuwa hakuna mifugo yoyote kutoka nchi jirani inayoingia au kuwekeshwa kwa mtu ye yote atakae kutwa anahifadhi mifugo hiyo atachukuliwa hatua za kisheria msigeuze Nchi yetu kuwa shamba la bibi, zoezi hili ni endelevu", alisema Mkuu huyo.

Aidha, Kanali Ndagala aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa kufanikisha zoezi hilo na kuwataka kuendelea kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa mifugo kutoka nje ya Nchi na kuwaagiza wananchi Wote wenye tabia ya kuwekeshwa mifugo kutoka Nchi jirani na kuajiri wageni kinyume na taratibu kuacha mara moja.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Gwanumpu Toi Butono alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wananchi kihifadhi Wahamiaji haramu pamoja na mifugo yao hali inayoweza kuongeza uhalifu katika kata hiyo kutokana na baadhi ya warundi wanaokaribishwa kujihusisha na vitendo viovu.

Hata hivyo aliwaomba Wananchi kuacha tabia hiyo na kuendelea kuzuia mifugo yao katika Wilaya hiyo ilikuweza kudumisha amani na usalama katika Kata hiyo.


That's an article KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO

Fine for article KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article KANALI NDAGALA AKAMATA NG'OMBE 93 NA RAIA WANNE WA BURUNDI KATIKA KIJIJI CHA BUKIRIRO With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/12/kanali-ndagala-akamata-ngombe-93-na.html

Subscribe to receive free email updates: