TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU - News Today in World

TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU

TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU
link : TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU

news-today.world |

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa taarifa ya makusanyo ya mapato ya kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2017, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.65. 

Makusanyo haya ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa  mwaka wa fedha 2016/17.
Katika kipindi hicho cha miezi mitatu, makusanyo ya kila mwezi yalikuwa kama ifuatavyo;-
Julai, 2017  Shilingi                        1,101,193,417,551.91
Agosti, 2017 Shilingi            1,205,008,256,053.51
Septemba, 2017 Shilingi    1,345, 339,916,757.65

Kwa makusanyo haya, Mamlaka ya Mapato Tanzania, inapenda kuwashukuru wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kwa kuendelea kulipa kodi na kuiwezesha serikali kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, Mamlaka inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki kwa kila mauzo na kudai risiti kwa kila manunuzi kwani ni njia pekee ya kupata mauzo sahihi yanayoiwezesha TRA kukokotoa kodi sahihi na kwa haki.

“Napenda kuwakumbusha wananchi wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wa tarehe na kiasi walicholipa na bidhaa waliyonunua kabla ya kuondoka na risiti hiyo. Endapo utaona haina vigezo tafadhali ripoti kwenye ofisi ya TRA iliyokaribu nawe au piga simu kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba 0800750075 au 0800780078. anasisitiza Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

Vile vile, Mamlaka inawakumbusha wamiliki wa majengo nchini kulipa kodi ya majengo mapema badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka wa fedha ili kuepuka misongamano na usumbufu usio wa lazima.

Pia, wafanyabiashara wa michezo ya kubahatisha wanapewa wito wa kulipakodi zao kwa mujibu wa sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41.


That's an article TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU

Fine for article TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.65 KIPINDI CHA JULAI - SEPTEMBA MWAKA HUU With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/10/tra-yakusanya-trilioni-365-kipindi-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :