RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN - News Today in World

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN
link : RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN

news-today.world |
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki kiongozi waJumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan wakiongea na wanahabari (hawapo pichani) mgeni huyo alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wa serikali katika picha ya pamoja na kiongozi waJumuiya ya Ismailia duniani H.H. Prince Karim al-Hussayni Aga Khan na ujumbe wake alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 11, 2017.
*********************
Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan amesema Jumuiya hiyo imedhamiria kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kupanua hospitali ya Aga Khan iliyopo Jijini Dar es Salaam na kujenga chuo kikuu kikubwa katika Afrika Mashariki, Mkoani Arusha.


Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan amesema hayo leo tarehe 11 Oktoba, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipofanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Amesema Upanuzi wa hospitali ya Aga Khan utahusisha kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa kutoka 72 vya sasa hadi kufikia vitanda 172, utaimarisha matibabu ya moyo na kansa na utaongeza ufundishaji wa madaktari na wataalamu wengine wa afya.

Kuhusu chuo kikuu kitakachojengwa Arusha, Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan amesema Jumuiya hiyo imedhamiria kujenga chuo kikuu kikubwa ambacho kitafundisha viongozi sio tu wa Tanzania na Afrika Mashariki, bali pia Afrika nzima ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo ya Afrika.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan kwa taasisi zake kutoa huduma za kijamii hapa nchini, lakini ametoa wito kwa taasisi hizo kupunguza gharama za huduma zake kwa wananchi ili wananchi waweze kumudu hasa ikizingatiwa kuwa zimekuwa zikipata msamaha wa kodi kutoka Serikalini.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo tayari kuendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano na Aga Khan na amemuomba kiongozi huyo kuendelea kupanua uwigo wa huduma za taasisi zake ikiwa ni pamoja na kuwekeza Mjini Dodoma yaliko makao makuu ya Serikali.

Kwa upande wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Aga Khan Mtukufu Karim Al-Hussaini amesema yeye haamini kuwa ni kipaumbele kwa vyombo vya habari kujikita katika masuala ya siasa na badala yake anaamini kuwa vyombo vya habari vina wajibu mpana zaidi wa kujikita katika masuala ya maendeleo hususani katika nchini zinazoendelea, na kwamba Aga Khan ipo katika mchakato wa kujikita katika wajibu huo kwa kuwa na waandishi wa habari na wachambuzi mahiri.


That's an article RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN

Fine for article RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article RAIS MAGUFULI AKUTANA NA AGA KHAN With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/10/rais-magufuli-akutana-na-aga-khan.html

Subscribe to receive free email updates: