MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA - News Today in World

MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA

MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA
link : MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA

news-today.world |
  Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akikagua ujenzi wa Barabara ya Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Wakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou Cunfei

 Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumza alipokagua ujenzi wa Barabara ya Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kulia ni Wakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou CunfeiWakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG ya China Zhou Cunfei akizungumzia wakati Zungu alipokagua ujenzi wa Barabara hiyo, leo.
 Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akihitimisha kwa kuzungumza na ujumbe wake baada ya kukagua ujenzi wa Barabara ya Olympio na ya Mtaa wa Mfaume, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam. 
*************************
Na Bashir Nkoromo
MBUNGE wa Ilala, Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu, amesema ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Barabara ya Olympio, katika kata Upanga Mashariki, huku akilalamikia ujenzi wa Barabara ya Mtaa wa Mfaume ambayo ujenzi wake umekwama.

Zungu amesema hayo leo alipokagua maendeleo ya ujuenzi wa barabara hizo ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami chini ya usimamizi na gharama za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

"Kama mnavyoiona, barabara hii ya Olympio inayojengwa na kampuni ya kigeni ya China Railway Seventh Group (CRSG), imejengwa kwa kiwango kizuri kabisa, lakini hii ya Mtaa wa Mfaume yenye urefu wa mita 900, ambayo mkandarasi wake ni kampuni ya CASCO abayo ni ya mzawa mwenzetu

imekwama kumalizika, Sasa tunamtafuta Mwenyekiti wa Halmashauri tujue nini hasa kimesababisha ujenzi wa barabara huu kukwama", amesema Zungu.

Amesema, wakati barabara ya Olympio yenye urefu wa mita 740  ujenzi wake umekamilika kwa kiwango kikubwa tangu Septemba 30, mwaka huu, ujenzi wa barabara ya  Mfaume umekwama hadi sasa kutokana na Mkandarasi kusimamishwa kuendelea kutokana na kuonekana anaijenga kwa viwango vya chini.

Wakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG Zhou Cunfei, alisema licha ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 95, kampuni hiyo inamalizia sehemu chache zilizobaki na inainatarajia kuikabidhi rasmi Januari 2, mwakani.


That's an article MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA

Fine for article MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article MUSSA ZUNGU AKAGUA MABORESHO YA BARABARA UPANGA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/10/mussa-zungu-akagua-maboresho-ya.html

Subscribe to receive free email updates: