WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU - News Today in World

WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU

WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU
link : WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU

news-today.world |
Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dodoma wakishirki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa Gaddafi Mjini Dodoma jana ambapo pamoja na mambo mengine waislamu waliaswa kudumisha amani na utulivu vilivyopo nchi na si kuleta machafuko. (Picha na Mroki Mroki).

Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dodoma wakishirki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa Gaddafi Mjini Dodoma jana ambapo pamoja na mambo mengine waislamu waliaswa kudumisha amani na utulivu vilivyopo nchi na si kuleta machafuko.

WATANZANIA wameaswa kuilinda na kudumisha amani iliyopo nchini na kamwe wasithubutu kushawishiwa na watu kuivuruga kwa namna yeyote ile. Anaandika Mroki Mroki-DAILY NEWS Digital.


Kauli hiyo imetolewa na Shehe na Kadhi mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shaaban wakati akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid El Hajj iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti Mkuu wa Gaddafi mjini Dodoma jana.

Shehe Shaaban alisema Tanzania kama mataifa mengi ya afrika yaliasisiwa na viongozi wetu kwa njia ya amani lakini hadi sasa mataifa mengi yameshavuruga amani yao na wanaishi maisha ya mashaka, hivyo alisema Watanzania hawanabudi kujivunia hali ya amani iliyopo pasipo kuivuruga. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


“Urithi wetu ni amani na utulivu nan i urithi wa umma wa waislamu dunia nzima hivyo hatuna budi kuendeleza na kudumisha upendo, amani na mashikamano katika familia zetu, jamii na hata kwa taifa kwa ujumla, kama ambavyo Mtume wetu, Muhamad (S.AW) alituhusia kufanya katika swala yake ya mwisho ya Hijja,” alisema Shehe Shaaban.

Aidha alisema amani ya nchi yetu na Afrika ni amani yenye historia kutoka kwa waasisi wa mataifa yetu akiwataja, Mwl. Julius Nyerere, Nelson Mandela, Kwame Nkruma, Mohamad Gaddafi, Jomo Kenyatta na wengine wengi.

Akitolea mfano wan chi ya Libya, Shehe Shaaban, alisema taifa hilo lilikuwa ni lenye amani na utajiri mkubwa Afrika lakini kutokana na kukubali chokochoko toka mataifa mengine waliamua kuvuruga amani yao na sasa wapo katika hali mbaya ya kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Shehe Shaaban amewaasa wakazui wa mkoa wa Dodoma kutitumia fursa ya ujio wa serikali na viongozi wake mjini Dodoma katika kujipatia maendeleo.

Alisema Maendeleo ya wana Dodoma hayanabudi kuletwa na wenyeji wenyewe kwanza na wasisubiri wageni ndio walete maendeleo.

Alizitaka taasisi za dini, mashirika na taasisi mbalimbali za mkoani Dodoma kuwekeza katika maeneo mbalimbali yakiwepo ya elimu, afya na viwanda ili kuleta maendeleo mkoani humo.
 Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dodoma wakishirki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa Gaddafi Mjini Dodoma jana ambapo pamoja na mambo mengine waislamu waliaswa kudumisha amani na utulivu vilivyopo nchi na si kuleta machafuko.
Waumini wa Dini ya Kiislamu walioshiriki katika Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa Gaddafi Mjini Dodoma jana wakisikiliza mawaidha kutoka kwa Shehe Mkuu na Kadhi wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shabaan (hayupo pichani) ambaye aliwaasa waislamu na watanzania wote kudumisha amani na utulivu vilivyopo nchi na si kuleta machafuko.
 Waumini wakiingia na kutoa zaka
Wengine walifanya na manunuzi ya kazu na baghakashea
 Wasichana Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiondoka katika viwanja vya Msikiti wa Gaddafi mjini Dodoma baada ya kushiriki Swala ya Eid El Hajj, iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti wa Gaddafi leo.
waumini wakipiga picha na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.


That's an article WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU

Fine for article WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article WATANZANIA WAASWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/09/watanzania-waaswa-kudumisha-amani-na.html

Subscribe to receive free email updates: