WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI - News Today in World

WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI

WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI
link : WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI

news-today.world |


Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering,Shin Soo akimueleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4. Kushoto ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale.



Mafundi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V wakiendelea na ujenzi wa moja kati ya madaraja makubwa saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.


Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) hatua mbalimbali za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), wakati Waziri huyo alipoikagua, mkoani Arusha.
Moja kati ya madaraja saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.



Tingatinga likiendelea na kazi ya ujenzi wa awali ya madaraja katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering,Shin Soo (katikati)alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4 jijini Arusha.
 *******************

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa wito kwa wakazi wa Arusha kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V ili kuweza kukamilisha kwa wakati ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.


Akikagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo mkoani humo, Profesa Mbarawa amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na hivyo kuvutia watalii na kukuza uchumi wa mkoa.

"Kukamilika kwa barabara hii ya Arusha bypass kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano kwani magari makubwa ya mizigo yatatumia mchepuo huu na kurahisisha huduma za usafirishaji jijini Arusha", amesema Waziri Mbarawa.

Ameongeza kuwa Wizara yake itasimamia kwa ukaribu ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa wakati uliopangwa na viwango vinavyostahili vilivyokubalika.

Aidha, Prof. Mbarawa ameupongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuitunza barabara hiyo ili idumu kwa muda uliopangwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Ven Ndyamukama, amesema Wizara kwa kushirikiana na TANROADS itaendelea kuhakikisha barabara na madaraja yote nchini yanajengwa kwa viwango vilivyopo kwenye usanifu wa kina (Detail design), na thamani ya fedha inapatikana.

Naye, Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili akamilishe mradi kwa wakati kama walivyokamilisha ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 na kwa ubora unaostahili.

Mhandisi Kalupale, ameeleza changamoto zinazoikabili barabara hiyo kuwa ni wingi wa  udongo wa tifutifu na  mfinyanzi na hivyo kulazimu Usanifu wa kina wa barabara hiyo kurudiwa upya.

Ujenzi wa Barabara ya Arusha bypass unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 67 ikiwa ni ushirikiano wa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na ujenzi wake utahusisha madaraja makubwa 7, maboksi kalvari 55 na madaraja ya bomba 55.


That's an article WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI

Fine for article WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/09/wakazi-wa-arusha-watakiwa-kutoa.html

Subscribe to receive free email updates: