UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF - News Today in World

UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF

UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF
link : UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF

news-today.world |
Wabunge wote wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni leo wamegoma kushiriki Kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Viti Maalum kutoka Chama cha CUF, ambao walikuwa wakiapishwa hii leo na Spika wa Bunge Job Ndugai wakati wa kuanza kwa kikao cha Bunge mjini Dodoma.
Wabunge wa upinzani wakiwa nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge wapya wa CUF.
Wabunge wapya wa CUF wakiwa katika nafasi zao Bungeni mjini Dodoma leo. baada ya kula kiapo. Wengine ni baadhi ya Wabunge wa CUF wasio fungamana na upande wa Kambi ya Upinzani.


Na Mroki Mroki, Dodoma
WABUNGE wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, leo waligoma kuhudhuria kuapishwa kwa Wabunge wapya wa viti maalum kutoka Chama cha wananchi CUF, kazi iliyofanyika Bungeni na kuongozwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.

Wakiwa wamevalia nguo nyeusi wabunge hao kutoka vyama vyote vya upinzani bungeni hata wale wa CUF walikuwa katika makundi nje ya Ukumbi wa Bunge katika jingo la zamani la Ukumbi wa Pius Msekwa.

Baadae baada ya kukamilika uapishaji wa wabunge wapya ndani ya ukumbi wa Bunge, waliandamana kwa pamoja hadi katika lango kuu la Bunge na kukusanyika kasha kuzungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi wao huo wa kugomea shughuli ya kuapisha Wabunge wapya wa kambi hiyo Bungeni.

Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Momba, kupitia Chama cha Demorasia na Maendeleo Chadema, David Silinde alizungumza na wanahabari na kusema kuwa wamefanya hivyo kuunga mkono wenzao waliofukuzwa na kufungua kesi Mahakamani.

Silinde alisema hawatawaunga mkono wala kushirikiana na wabunge hao wapya wa CUF hadi Kesi ya Msingi iliyopo Mahakamani itakapo kamilika.

“Tumefanya hivi na tutaendelea na msimamo wetu wa kutoshirikiana na wabunge hawa hadi pale kesi ya Msingi itakapoisha Mahakamani,” amesema Silinde.


That's an article UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF

Fine for article UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article UPINZANI BUNGENI WAGOMEA KUSHIRIKI KUAPISHWA WABUNGE WAPYA WA CUF With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/09/upinzani-bungeni-wagomea-kushiriki.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :