JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI
JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post
Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.
Title : JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI
link : JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI
You are now reading the article JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/09/jafo-serikali-kukarabati-vituo-vya-afya.html
Title : JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI
link : JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI
news-today.world |
Na. Atley Kuni- TAMISEMI
Na. Atley Kuni- TAMISEMI
Serikali imepanga kukarabati vituo vya afya 172 kutokana na fedha kutoka Benki ya Dunia na Ubalozi wa Canada ambapo wametoa jumla ya Dolla za Kimarekani Mil 88 sambamba na Bil.12 fedha za kitanzania zilizovuka katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo (Mb) amesema lengo la serikali nikuhakikisha ifikapo Desemba 30, mwaka huu shughuli hiyo iwe imekamilika ipasavyo kwa kusimamiwa karibu na Wakuu wa mikoa wakisaidiana na Wakuu wa Wilaya.
Jafo amesema kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Serikali imepokea Dolla za kimarekani Mil. 66 kutoka Benki ya Dunia ambapo vituo 103 vitakarabatiwa aidha pia Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, imepata Msaada kutoka Ubalozi wa Canada wa dolla za kimarekani Mil 22, ambapo vituo 44 vya afya vitakarabatiwa kwa fedha hizo.
Naibu waziri huyo alisema, fedha zingine zitakazo tumika katika zoezi hilo ni zile zilizo vuka katika mwaka wa fedha uliopita.
“Vituo 25 vitafanyiwa ukarabati kupitia fedha za Benki ya Dunia na mfuko wa afya wa pamoja zilizovuka mwaka wa 2016/2017, ambapo Bil.12 za kitanzania zitatumika,” alisema Jafo na kuongeza kwamba kila “kituo kitapatiwa shilingi Mil. 500 za kitanzania na baada ya ukarabati serikali itakuwa na jukumu lakupeka vifaa katika maeneo hayo”.
Waziri Jafo amesema, Maeneo ya kipaumbele wakati wa ukarabati huo ni pamoja na Upasuaji (Theater), Wodi za mama na Mtoto (Martenity), Maabara(Laboratory), pamja na Nyumba za watumishi sambamba na maeneo mengine ya kipaumbele kutokana na fedha zilizopo.
Katika hatua nyingine Jafo amewagiza Makatibu Tawala wa mikoa kuwasilisha Taarifa ya kila mwezi ofisini kwake juu ya maendeleo ya ukarabati, huku akiwataka Wakurugenzi na watendaji wengine kusimamia kwa ufasaha zoezi hilo.
Naibu Waziri hakusita kuonya juu wale wote watakao kwenda kinyume na maagizo na maelekezo ya serikali yaliyotolewa
“Nawaomba Wabunge na Madiwani kushirikiana bega kwa bega na watendaji katika kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi, alisema Jafo na kuongeza kwamba, “ofisi yangu haita mvumilia Kiongozi au Mtendaji yeyote atakaye onekana kutumia fedha hizo vibaya au kushindwa kutimiza wajibu wake na kisha kukwamisha shughuli hii muhimu yenye nia njema kwa maisha ya watanzania.
Akihitimisha maagizo hayo Naibu waziri Suleima Jafo, amezishukuru Wizara zote za kisekta katika kusukuma gurudumu la maendeleo na kwenda sambamba na kasi ya Rais Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU, ikiwapo, Wizara ya Afya, Fedha na Mipango pamoja na watendaji wa Ofisi yake ambao walikuwa bega kwa bega katika mchakato wote wa kupatikana kwa fedha.
That's an article JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI
Fine for article JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.
You are now reading the article JAFO: SERIKALI KUKARABATI VITUO VYA AFYA 172 KWA FEDHA ZA WAHISANI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/09/jafo-serikali-kukarabati-vituo-vya-afya.html