POLISI YAUWA 13 KIBITI - News Today in World

POLISI YAUWA 13 KIBITI

POLISI YAUWA 13 KIBITI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title POLISI YAUWA 13 KIBITI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : POLISI YAUWA 13 KIBITI
link : POLISI YAUWA 13 KIBITI

news-today.world |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Chini ni silaha  8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro  akionesha makasha ya risasi (magazine) ambazo  ni miongoni  mwa makasha 8 yaliyokuwa yakitumiwa na wahalifu  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto  ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na  Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao walikuwa wakifanya mauaji  Kibiti.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro  akielezea  baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu  13 waliouawa  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti   ambapo  jumla ya  silaha 8 aina ya SMG,  risasi  158, pikipiki 2, pamoja na  begi la nguo  vilivyokuwa  vikitumiwa na wahalifu hao.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  akionesha silaha aina ya SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8  zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kulia  ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na  Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  akiongea na wananchi wa Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka kukagua eneo la tukio walipouawa  wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi  katika eneo la Tangibovu. – Picha na Jeshi La Polisi


That's an article POLISI YAUWA 13 KIBITI

Fine for article POLISI YAUWA 13 KIBITI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article POLISI YAUWA 13 KIBITI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/08/polisi-yauwa-13-kibiti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :