MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE - News Today in World

MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE

MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE
link : MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE

news-today.world |
Mahujaji kutoka sehemu mbalimbali nchini takribani 100 ambao wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam kwenda hija wakiwa uwanjani hapo usiku huu pasipo kujua hatma ya safari yao hiyo ya kwenda kutimiza ibada ya Hija, katika Mtakatifu wa Makkah, Saud Arabia baada ya kudai kutapeliwa na waliokuwa wakiratibu safari yao kupitia taasisi za  Taiba Hajj & Umrah Social Service Trust na Jamarat Hajj and Umrah Traveller (Picha na Katuma Masamba).
Mahujaji kutoka sehemu mbalimbali nchini takribani 100 ambao wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam kwenda hija wakiwa uwanjani hapo usiku huu pasipo kujua hatma ya safari yao hiyo ya kwenda kutimiza ibada ya Hija, katika Mtakatifu wa Makkah, Saud Arabia baada ya kudai kutapeliwa na waliokuwa wakiratibu safari yao kupitia taasisi za Taiba Hajj & Umrah Social Service Trust na Jamarat Hajj and Umrah Traveller
MAHUJAJI takribani 100 wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jiji Dar es Salaam  kwenda kufanya Hijja katika mji Mtakatifu wa Makka kutokana na taasisi zilizotakiwa kuwasafirishwa kushindwa kufanya hivyo. Anaandika Katuma Masamba.

Mahujaji hao ambao walitakiwa kuondoka leo wameshindwa kuondoka baada ya kuwepo sintofahamu huku viongozi wa Taasisi ya Taiba Hajj & Umrah Social Service Trust na Jamarat Hajj and Umrah Traveller hali iliyowafanya mahujaji hao kutofahamu hatma yao.

Akizungumza na TSN Digital uwanja hapa, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir  amewataka Mahujaji hao kuwa na subira wakati wakitafuta namna ya wao kuweza kusafiri ka ajili ya kwenda kutekeleza Ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika Nguzo za Kiislamu.

"Kipindi hiki mpaka kesho tunatarajia kupata majibu yoyote kutokana juhudi za viongozi, naomba mstahamili  tufanye subira tuone tutafikia wapi...mimi nitaendelea kufuatilia kuona safari inakamilika kiasi gani kupitia viongozi, kuna wengine hatujawapata hadi sasa lakini tunawatafuta," amesema Mufti.

Aidha, amewatoa hofu Mahujaji hao kuwa mipaka ya Mji wa Makka kufungwa usiku wa kuamkia Jumapili, hivyo muda bado upo wa kuweza kupata safari na kuwataka mahujaji hao kufanya dua na kumuomba Mungu ili waweze kutekeleze ibada hiyo.

Akizungumzia hatua ya kutekelezwa uwanjani hapo, Hussein Said Seif ambaye ametokea mkoani Mwanza amesema alilipa Sh milioni 8.5 kwa taasisi ta Taibah ili aweze kutekeleza ibada hiyo lakini hadi usiku hakuna jambo linaloeleweka ambapo ameshauri serikali kuchukua hatua dhidi ya taasisi za aina hiyo.

Naye, Ummy Sekibo  mkazi wa Dar es Salaam amesema, hali imewasikitisha wananchi na waislamu wote kwa ujumla kwani kitendo hicho si jambo jema na kwamba taasisi hiyo inapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo ya kufutiwa usajili wake.


That's an article MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE

Fine for article MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article MAHUJAJI WAPATAO 100 WAKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/08/mahujaji-wapatao-100-wakwama-uwanja-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :