WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI - News Today in World

WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI

WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI
link : WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI

newstoday-ok.blogspot.com ~
NAIBU Waziri  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amewahimiza watanzania kutumia kikoa(domain) ya tz jambo ambalo litachangia ukuaji wa uchumi. Anaandika Anastazia Anyimika.
 Akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa la watoa huduma za mitandao wa intaneti kwa Afrika ambao tanzania ni mwenyeji alisema kwa sasa Tanzania iko nyuma sana kwa kuwa na rajisi ya watumiaji 14,000 kati ya watanzania mililoni 45.

Alisema kwa watanzania kujiunga na kikoa (.Tz) kutaisadia wafanyabishara na wajasiliamali kufanya biashara zao na kukuza uchumi wa nchi.

Alisema kutokana na uchache wa watumiaji lunaifanya serikali kutoa ruzugu ya kuendesha kikoa hicho na kuwa jinsi watu wengi wanavyojiunga, ndipo gharama za wanaojiunga zinaweza kupungua. 

Aidha, Ngonyani alisema kwa  sasa gharama za interneti zimepungua kwa asilimia 50 baada ya kukamilika mkonga wa taifa wa mawasiliano.

Naye  Makamu wa Rais wa taasisi ya Afrika ya kikoa(Africa Top Level Domains organisation-AfTLD) Ali Hadji Mmadi alisema kwa sasa Afrika inawatumiaji miloni 2.9 kati ya wananchi bilioni moja wa bara hili.

"Miaka ya nyuma watumiaji wa domain walikuwa mililoni moja na wamepanda hadi kufikia mililoni 2.9, idadi hii ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watu," alisema.
Naye Meneja Maendeleo wa Afrika, Michuki Mwangi alisisitiza kila wananchi katika nchi za Afrika kutumia kikoa chao na kuwa na sera rafiki za kuwaongoza watumiaji wa interneti.
Mwenyekiti wa Watoa huduma za Intaneti nchini Tanzania (TISPA), Erik Rowberg akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo na kuwahimiza watanzania kutumia kikoa cha tz kwani ni kitambulisho peke cha utaifa wao kwani hata yeye anajivunia kutumia kikoa hicho cha .tz katika tovuti yake ya www.habari.co.tz.
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo la tano la
Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA), Dkt, Raynold Mtungahema akizungumza wakati wa ufunguzi huo.
 Washiriki wakifuatilia mkutano huo.
 NAIBU Waziri  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani akizungumza wakati akifafanua jambo kwa wanahabari.
 Waratimu wa Mkutano huo wakizungumza na waandishi wa habari.
 Mijadala mbalimbali ikiendelea.
 washiriki wakifuatilia mijadala
 Mijadala ikiendelea ...
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani(walioketi katikati) na waratibu wa kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali za Afrika.


That's an article WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI

Fine for article WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article WATANZANIA TUMIENI KIKOA CHA tz KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/watanzania-tumieni-kikoa-cha-tz.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :