WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI - News Today in World

WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI

WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI
link : WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI

newstoday-ok.blogspot.com ~

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanachama na wadau wa timu ya lipuli kwenye mkutano wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa timu ya lipuli uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Mwembetogwa.

Baadhi ya wadau na wanachama wa timu ya lipuli wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo bi Asia Abdallah
*******************
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa,  Asia Abdallah aliwataka wananchi wa Mkoa wa Iringa kuishi bila kuwa na majungu kwa sababu majungu yanarudisha nyuma maendeleo.

Hayo yamesemwa wakati wa hotuba ya uchaguzi wa kuwapa viongozi wapya wa timu ya Lipuli katika ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa ulipo Manispaa ya Iringa.

Asia alisema kuwa Iringa kumekuwa na majungu ambayo yamekuwa yakileta uchonganishi baina ya watu na watu pia viongozi na viongozi hivyo inatakuwa kubadilika na tusiishi kwa mazoea.

"Ukiiinga huku majungu kule majungu hasa mtu hana pesa ya kula lakini anashinda kwenye mitandao ya kijamii kuleta majungu,fanyeni kazi kwa nguvu zenu zote maana mnaendekeza tu majungu ambayo hayana manufaa kwako binafsi hata taifa kwa ujumla"alisema Asia.
Aidha Asia alisema kuwa viongozi wa timu ya lipuli watakaoingia madarakani kuhakikisha wanavunga makundi yote ya majungu na kuhakikisha timu inakuwa na umoja na ushirikiano kila nyanja ili kupata mafanikio makubwa ambaya yataleta faraja kwa wakazi wa Iringa na wapenda Soka.

"Haiwezikani kila kona ni majungu tu hivi nyie hamna kazi za kufanya tena afadhali wanawake wangekuwa na majungu lakini majungu hayo yanaongozwa na wanaume kwenye magroup ya what's up,achaneni na magroup ambayo hayana faida kwako wala hanaya afya kwa taifa la Tanzania" alisema Asia.

Mohammed aliongeza kwa kusema kuwa Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli anahimiza wananchi kufanya kazi na sio kutengeneza majungu ambayo yamekuwa yakikwamisha maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Soka Mkoani Iringa Dr Ally Ngalla alimshukuru Mkuu wa wilaya huyo kwa hotuba nzuri na kumuahidi kuwa Iringa itabadilika na kufuta majungu kutokana na tayari wamepata viongozi wapya wa timu ya lipuli.

"Nikiwa kama kiongozi nitahakikisha makundi yote ya majungu yanavunjwa na kuwa kitu kimoja ambapo tutafanya kazi kama siafu ili kuinua Mpira wa miguu Mkoani Iringa "alisema Ngalla

Ngalla aliwata wadau wa mpira miguu Mkoani Iringa kusahau yaliyopita na kuangalia nini cha kufanya ili kuisadia timu ya lipuli ifanye vizuri kwenye ligi kuu Tanzania bara na kulejesha furaha ya wananchi wa Iringa.

Naye Mwenyekiti Mpya wa timu ya lipuli Ramadhani Mahano aliwaomba wadau wa Mpira na wapenzi wa timu ya lipuli kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja kuvunja makundi yote yaliyokuwa yanasababisha migogoro ya lipuli na Mpira wa miguu kwa ujumla.

Nawaombeni sana kuyaka kichwani vizuri maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Kilolo bi Asia Abdallah kwa kuacha majungu au kusababisha migogoro ambayo haina maana bali naomba tushauriane kwa kila jambo kwa manufaa ya lipuli na wadau wa mpira.


That's an article WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI

Fine for article WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUACHA MAJUNGU WAFANYE KAZI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/wananchi-iringa-watakiwa-kuacha-majungu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :