VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA - News Today in World

VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA

VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA
link : VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA

newstoday-ok.blogspot.com ~
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (wa tatu kutoka kulia) akimweleza jambo Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (wa kwanza kutoka kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, unaojulikana kama Murongo-Kikagati. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano. Wengine pichani ni Maofisa mbalimbali kutoka TANESCO, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Ardhi.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt.  Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda (wa pili kutoka kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 35 wa Nsongezi kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwebangi Luteganya, Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni Makala na Meneja wa Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka TANESCO, Mwesiga Mwesigwa.



Meneja wa Uwekezaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Rwebangi Luteganya (kushoto), akiwaeleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt.  Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano (kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 35 wa Nsongezi kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda.



Sehemu ya Mto Kagera, unavyoonekana katika eneo la Nsongezi, mpakani mwa Tanzania na Uganda. Maji ya Mto huo yatatumika kuzalisha umeme wa megawati 35 kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya wananchi wake. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.




Sehemu ya viongozi na wataalam mbalimbali kutoka Tanzania, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt.  Juliana Pallangyo (wa pili kutoka kushoto), wakitoka kukagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, unaojulikana kama Murongo-Kikagati.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.Juliana Pallangyo (katikati), akisaini Kitabu cha Wageni katika Kituo cha Forodha Murongo, kilichopo mpakani mwa Tanzania na Uganda, alipokuwa katika ziara ya kazi kukagua maeneo itakapotekelezwa Miradi ya umeme kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera, Francis Maze na kulia ni Ofisa Mfawidhi wa Kituo hicho cha Forodha, Ezekia Nonkwe.
                                           *****************
Na Veronica Simba – Kagera
Baadhi ya viongozi na maofisa mbalimbali wa Serikali ya Tanzania, wamefanya ziara ya siku moja mpakani mwa Tanzania na Uganda, katika maeneo ya Nsongezi, Murongo na Kikagati, kwa ajili ya kukagua maeneo inapotarajiwa kutekelezwa miradi ya sekta ya nishati inayohusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt.Juliana Pallangyo, imefanyika leo Julai 27 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Tanzania na Uganda kuhusu ushirikiano kwenye masuala ya mpakani, unaotarajiwa kufanyika Julai 29, wilayani Bukoba Mkoa wa Kagera.

Kiongozi mwingine wa Serikali aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu Pallangyo katika ziara hiyo ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano.

Kwa mujibu wa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera, Francis Maze, miradi ya ushirikiano kwa sekta ya Nishati kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda inahusisha Mradi wa kuzalisha umeme wa Murongo-Kikagati wenye megawati 14, Mradi wa kuzalisha umeme wa Nsongezi wa megawati 35 pamoja na Mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vya mpakani mwa nchi hizo mbili.

Mkutano wa Mawaziri wa Tanzania na Uganda utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kutoka nchi hizo mbili wanaoshughulika na masuala ya ushirikiano katika maeneo ya Mpaka, uliopangwa kufanyika kesho, Julai 28.

Maofisa wengine wa Serikali walioshiriki ziara ya kukagua maeneo itakapotekelezwa miradi ya nishati ni pamoja na Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwebangi Luteganya, Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni Makala, Meneja wa Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka TANESCO, Mwesiga Mwesigwa na Mtaalam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Raymond Bagenda.


That's an article VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA

Fine for article VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article VIONGOZI TANZANIA WAKAGUA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA TANZANIA NA UGANDA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/viongozi-tanzania-wakagua-maeneo-ya.html

Subscribe to receive free email updates: