RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE - News Today in World

RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE

RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE
link : RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE

newstoday-ok.blogspot.com ~
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe kufuatia kifo cha mkewe Bi. Linah George Mwakyembe kilichotokea usiku wa tarehe 15 Julai, 2017.

Bi. Linah George Mwakyembe amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, na amesema yeye na familia yake wanaungana na familia ya Dkt. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Nakupa pole sana Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amesali Ibada ya Jumapili ya 15 ya mwaka wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita na ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.

Katika harambee hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amefanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 13, ahadi Shilingi 920,000/=, mifuko ya saruji 33 na malori 2 ya mchanga.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza waumini wa Parokia ya Chato kwa hatua kubwa waliyopiga katika ujenzi wa kanisa kuu la Parokia hiyo na amewataka kuendelea kujitolea kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi huo.


That's an article RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE

Fine for article RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article RAIS MAGUFULI AMFARIJI WAZIRI MWAKYEMBE With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/rais-magufuli-amfariji-waziri-mwakyembe.html

Subscribe to receive free email updates: