KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU
KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post
Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.
Title : KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU
link : KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU
You are now reading the article KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/kingu-atatua-kero-za-afya-jimbo-la-lissu.html
Title : KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU
link : KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU
news-today.world |
MBUNGE wa Singida Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu amewafuta machozi akinamama wa jimbo jirani la Singida Mashariki linaloongozwa na Tundu Lissu wilayani Ikungi, Singida baada ya kuwanunulia vitanda 52 ili kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto. Anaandika Mroki Mroki/TSN Digital DSM.
Kwa muda mrefu, akinamama hao walikuwa na kilio cha kukosekana kwa huduma hizo, hasa vitanda vya kujifungulia, hivyo kumlilia Kingu aliyeamua kubeba jukumu na mbunge mwenzake.
Akizungumza na TSN Digital kwa njia simu, Kingu alisema ameamua kutoa msaada huo kutokana na maombi aliyoyapata kutoka kwa akinamama wa eneo la Ikungi na pia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida juu ya kuwasaidia katika sekta ya afya kwa kuwapatia vitanda vya kujifungulia.
“Ni kweli ninatarajia siku yoyote nitakwenda kukabidhi vitanda 86 katika Wilaya ya Ikungi, ambako kuna majimbo ya Singida Magharibi nilipo mimi na jimbo jirani la Singida Mashariki kwa Tundu Lissu, kufuatia maombi ya wananchi hasa akina mama ambao huteseka sana kwa kwenda umbali mrefu kutafuta huduma za afya wakati wa kujifungua,” alisema Kingu.
Kingu alisema kati ya vitanda hivyo 86 vyenye thamani ya Sh. Milioni 48.9, vitanda 52 atavigawa katika jimbo la Singida Mashariki na vingine 34 atavigawa katika jimbo lake la Singida Magharibi.
Amesema kati ya vitanda hivyo 52 atakavyovigawa Singida Mashariki, vitanda 26 ni maalumu kwa ajili ya akinamama kujifungulia na vitanda vingine 26 kwa ajili ya wodi za kawaida.
Aidha, amesema katika jimbo lake atakabidhi vitanda 34 vya kujifungulia ambavyo kati ya hivyo, vitanda vinne ni vya kisasa vinavyotumia umeme.
Wilaya ya Ikungi ina jumla ya Kata 28 ambapo kati ya hizo, kata 13 zipo katika jimbo la Singida Mashariki ambapo katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya hiyo ilikuwa na takribani wakazi 272,959.
That's an article KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU
Fine for article KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.
You are now reading the article KINGU ATATUA KERO ZA AFYA JIMBO LA LISSU With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/kingu-atatua-kero-za-afya-jimbo-la-lissu.html