IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO - News Today in World

IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO

IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO
link : IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO

news-today.world |

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo na kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya sheria na taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali kwa watendaji wa Jeshi hilo hatua ambayo italiwezesha kufanyakazi zake kwa weledi katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.

IGP Sirro, amefanya ziara hiyo ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na maofisa ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.

Katika mazungumzo yake IGP Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza wajibu wao kwa kutenda haki na bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.

Hata hivyo, katika mabaraza ya kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya hoja kadhaa ziliibuliwa kwa baadhi ya askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, ambapo IGP Sirro aliahidi kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Aidha, katika ziara yake IGP Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na mbinu na mikakati ikijadiliwa katika kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.


That's an article IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO

Fine for article IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KISHINDO With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/07/igp-sirro-amaliza-ziara-yake-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :