WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI
WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post
Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.
Title : WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI
link : WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI
You are now reading the article WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/wanne-wauwawa-katika-mapambano-na.html
Title : WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI
link : WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI
newstoday-ok.blogspot.com ~
Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas akionesha moja ya silaha zilizopatikana katika mapambano hayo.
**************
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani. Anaandika Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.
Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.
“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.
Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
That's an article WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI
Fine for article WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.
You are now reading the article WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/wanne-wauwawa-katika-mapambano-na.html