RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA - News Today in World

RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA

RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA
link : RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA

newstoday-ok.blogspot.com ~

KUFUATIA Kifo cha Shabiki maarufu wa Klabu ya Yanga, Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Chama cha Mapinduzi (CCM) Ali Yanga, Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa wote waliofikwa na msiba huo.

Rais Magufuli ametma salamu hizo leo kwa familia ya marehemu, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uongozi wa Klabu ya Yanga na wanamichezo wote kwa ujumla kufuatia kifo cha shabiki mkubwa wa timu ya Yanga  Ali Mohamed maarufu kwa jina la Ali Yanga.

Ali Yanga amefariki dunia jana jana Juni 20, 2017 kwa ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Chipogolo kilichopo katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Rais Magufuli atamkumbuka Ali Yanga kwa uzalendo wake na mchango wake wa kuhamasisha na kushabikia masuala mbalimbali ya kitaifa na hasa michezo, ikiwemo kuishabikia timu yake ya Yanga, timu ya soka ya Taifa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na shughuli za kiserikali kama vile Mwenge wa Uhuru na ziara za viongozi.

“Nimeguswa sana na kifo cha Ali Yanga, nilikuwa nae wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo alitoa mchango mkubwa katika uhamasishaji wa wananchi kukipigia kura chama changu cha CCM, na pia amekuwa akiongoza mashabiki wenzake kuishabikia timu ya Yanga na timu ya Taifa bila kuchoka. Kwa kweli alikuwa hodari sana katika ushabiki wake.

“Natoa pole nyingi sana kwa familia yake, viongozi wa timu ya Yanga, wanamichezo wote, wana CCM na wote walioguswa na kifo cha Ali Yanga na namuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina” amesema  Rais Magufuli.


That's an article RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA

Fine for article RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article RAIS MAGUFULI AMLILIA ALI YANGA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/rais-magufuli-amlilia-ali-yanga.html

Subscribe to receive free email updates: