POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI - News Today in World

POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI

POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI
link : POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI

newstoday-ok.blogspot.com ~

JESHI la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya uhalifu klatika siku ya siku kuu ya Eid El Fitri.

Taariofa iliyotolewa na Jeshi hilo kupitia kwa Msemaji wake Advera Bulimba imewataka  wananchi kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao.   

"Kipindi kama hiki cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu na vitendo vingine ambavyo huhatarisha usalama wa watu na mali zao,"ilisema taarifa hiyo.

Naibu kamishna huyo wa Polisi, Advera Bulimba alisema Jeshi la Polisi nchini,  limejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwamba  wananchi wanasherehekea Sikukuu katika hali ya amani  na utulivu.  

Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu. 

"Vilevile,  Jeshi la Polisi linawatahadharisha watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kuwa makini  na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani,  Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaovunja  sheria na kanuni za usalama barabarani kwa mabereva kutumia vilevi, bodaboda kubeba  mishikaki, kwenda mwendo kasi pamoja na kupiga honi hovyo," taarifa hiyo ilieleza.

Pia, tunawataka  wananchi wote kuwa wepesi katika  kutoa taarifa kwa kupitia  namba za simu za bure 111 au 112  pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara.


That's an article POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI

Fine for article POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article POLISI YATOA TAHADHARI KWA WAHALIFU SIKU YA EID EL FITRI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/polisi-yatoa-tahadhari-kwa-wahalifu.html

Subscribe to receive free email updates: