MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA
MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post
Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.
Title : MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA
link : MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA
You are now reading the article MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-samia-awataka-wapelelezi.html
Title : MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA
link : MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA
newstoday-ok.blogspot.com ~
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewaagiza wapelelezi na waendesha mashtaka nchini waepukane na vitendo vya rushwa bali wafanye kazi kwa bidii kwa kuweka maslahi ya taifa mbele kwa kuchukua hatua stahiki watu wanaoiba rasilimali za Taifa.
Makamu wa Rais, Samia ametoa kauli hiyo wakati anazindua mwongozo kwa wapelelezi na waendesha mashtaka wa kesi za wanyamapori na misitu katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Jijini Dar es Salaam.
Amesema mwongozo aliouzindua utasaidia kwa kiwango kikubwa uboreshwaji wa upelelezi na uendeshaji wa kesi zinazohusu wanyapori na misitu nchini.
“Uwepo wa mwongozo huu ni dhahiri unategemewa kutoa matokeo chanya katika mapambano dhidi ya ujangili na uhalifu misitu yetu” Amesisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa anaimani mwongozo huo aliouzindua utasaidia kukomesha vitendo uhalifu ambavyo vimekuwa vikilisababishia Serikali hasara kubwa ikiwemo uharibifu wa rasilimali za taifa na kupoteza mapato ambayo yangesaidia kuimarisha huduma za kijamii nchini.
Kuhusu sekta ya utalii nchini, Makamu wa Rais amesema pamoja na sekta hiyo kuliingizia taifa mapato mazuri lakini inasikitisha kuona kuwa uwepo wa wanyamapori ambao ndio nguzo kuu ya sekta ya utalii unazidi kupungua kila kukicha hivyo kuwa tishio kubwa kwa uchumi na nchi.
Amesema vitendo vya ujangili vimeendelea kuangamiza wanyama hasa tembo hivyo ni muhimu kwa wapelelezi na waendesha mashtaka kutenda haki bila kuonea mtu kwa watu wanaokamatwa kufanya vitendo hivyo ili viweze kukomeshwa nchini.
“Wazee wetu walilinda na kutunza rasilimali zetu kwa faida yetu nasi tuzitunze kwa ajili ya vizazi vijavyo” Ameeleza Makamu wa Rais
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa kazi ya kupambana na ujangili na utoroshaji holela wa wanyama na viumbe wengine itakuwa endelevu na wale wote watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Waziri Profesa Maghembe amemwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini kuendesha oparesheni ya maalum ya kukusanya silaha zote ambazo zimekuwa zikitumika kwenye ujangili ili kuhakikisha wanyama hasa tembo wanakuwa salama kwenye maeneo ya Hifadhi za Taifa nchini.
Naye, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga amefafanua kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2017 ofisi yake imewafikisha mahakamani washtakiwa wakubwa wa ujangili ambao walikuhumiwa vifungo virefu na faini.
Amesema kuwa washtakiwa 100 walihukumiwa kulipa faini ya zaidi ya shilingi bilioni 1.1 kwa kujihusisha na nyara za Serikali kinyume na sheria na faini hizo zimehalipwa Serikali.
Ameeleza kuwa kati ya idadi hiyo watuhumiwa zaidi ya 80 walihukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 30 gerezani na faini ya zaidi ya shilingi milioni 164 ambazo bado hazijalipwa Serikalini.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga amesema mafanikio hayo yote yamechangiwa na usimamizi madhubuti wa kesi hizo kupitia dawati la wanyamapori katika Divisheni ya Mashtaka pamoja na Mawakili wa Serikali katika Ofisi zote za mikoani nchini.
Ameeleza kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo kwenye kazi kwa sasa ni dhamana kwa watuhumiwa wakubwa wa vitendo vya ujangili ambapo utafiti uliofanywa Mahakama za mkoa wa Dar es salaam tu katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 unaonyesha kuwapo kwa jumla ya mashauri 13 yanayohusishwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 800 zilizokamatwa ndani na nje ya nchi ambapo watuhumiwa wake walipewa dhamana na kutoweka.
Biswalo Mganga amesema katika mashauri hayo asilimia 69 walikuwa ni raia wa kigeni na asilimia 31 ni raia wa Tanzania.
That's an article MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA
Fine for article MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.
You are now reading the article MAKAMU WA RAIS SAMIA AWATAKA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA KUEPUKA KUEPUKA RUSHWA With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-samia-awataka-wapelelezi.html