JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI - News Today in World

JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI

JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI
link : JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI

newstoday-ok.blogspot.com ~

 MMOJA wa askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko) mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro 833KJ Arusha ,akionesha umahiri na ukakamavu wake kwa kuzuia pikipiki isiondoke kwa mikono.
 Baadhi ya askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko) mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro 833KJ Arusha ,wakionesha umahiri na ukakamavu wao kwa kupitiwa na pikipiki juu ya migongo yao.

 Baadhi ya askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko) mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro 833KJ Arusha ,wakionesha umahiri na ukakamavu wao kwa kukunja kipande cha nondo yenye ujazo wa milimita 16 kwa mikono.
 Baadhi ya askari wapya wa JWTZ Kundi la 37 la Mwaka 2016 lililopikwa kwa Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko) mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro 833KJ Arusha ,wakionesha umahiri na ukakamavu wao.
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema nia ya kuongeza uandikishaji wa vijana wenye elimu ya juu jeshini unalenga kuwa na askari wenye uwezo mkubwa wa kutafsiri mambo haraka.

Hayo yalielezwa na  Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Uongozi Monduli (TMA), Meja Generali Paul Masao alipokuwa akifunga mafunzo ya askari 1,833.

Kundi hilo la 37 la Mwaka 2016 lilipikwa kwa Wiki 18 katika Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS Kihangaiko) mkoani Pwani, kisha kufunga mafunzo yao Uwanja wa Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro 833KJ.

Akizungumza baada ya gwaride la mwendo wa pole na haraka kutoa heshima, maonyesho ya askari waliohitimu na kula kiapo cha utii Meja Generali Masao aliwataka wahitimu hao kuitumia elimu ya juu kama chachu ndani ya JWTZ.

“Nia ya JWTZ kuongeza uandikishaji wa askari wenye elimu ya juu ni kuwezesha uwapo wa askari wenye elimu ya kuwawezesha kutafsiri mambo haraka,” alisema Meja Generali Masao na kuongeza:

“Elimu mliyonayo ikawe chachu ndani ya jeshi,ikalete matokeo chanya kazini.Isibakie kuandikisha wasomi wasiokuwa na matunda.Tunataka kuona elimu ikisaidia kufungua wigo wa uelewa kwa wanajeshi wetu,” alisema.

Aidha aliwataka askari hao kujiepusha na matumizi ya nguvu migogoro kati yao na raia, ikiwamo marufuku kujihusisha na vikundi vya dawa za kulevya, bangi, unyanyasaji na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

“Itumieni kwa busara mitandao ya kijamii si kwamba hatutaki muitumie lakini wanajeshi siku zote tuna akiba ya maneno kwani tunaongozwa na miiko yetu.

“Tukikubaini dhidi ya vitendo hivi utakuwa umepoteza sifa jeshini na utafukuzwa. Niwasihi jiendelezeni kielimu fanyeni mambo ya kimaendeleo ili kuepuka kudhalilika wakati wa kustaafu,” alisema

Meja Generali Masao alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha askari hao jukumu lililombele yao la kulinda nchi dhidi ya maadui wa ndani na nje, ikiwamo kusaidia majanga ya kitaifa na kimataifa watakapohitajika.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya awali ya Kijeshi, RTS Kihangaiko Kanali Chilo Okombo alisema kuwa askari hao 1,833 wamefanya vizuri katika masomo yao huku askari 6 wakishindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali.

Naye Kamanda Kikosi cha 833 KJ Oljoro Luteni Kanali Sijaona Myala aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanazingatia mambo ya msingi ambayo ni utii, uhodari na kuheshimu sheria.

Mbali ya kuhudhuriwa na maofisa mbalimbali wa jeshi sherehe hizo zilihudhuriwa pia na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini waliofika kushuhudia ndugu na jamaa zao wakihitimisha mafunzo ya awali ya kijeshi.


That's an article JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI

Fine for article JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article JWTZ LAELEZA SABABU YA KUANDIKISHA WASOMI WENGI JESHINI With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/jwtz-laeleza-sababu-ya-kuandikisha.html

Subscribe to receive free email updates: