BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF - News Today in World

BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF

BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF - Hallo World !!! News Today in World, In this article you read by title BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF, We've prepared this article well so you can read and retrieve information on it. Hopefully the contents of the post Article DAILY NEWS-HABARILEO, What we write can you understand. Okay, happy reading.


Title : BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF
link : BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF

newstoday-ok.blogspot.com ~

MBIO za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard (pichani juu) kujitosa kuwania urais wa shirikisho hilo.

Shija ambaye ni Meneja ndani TRA, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado.

“Ni kweli nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi kuhusu mimi na kwa nini nimejitosa katika nafasi hii, tuvute subira wakati wa kampeni ukifika nitazungumza, ila kwa leo itoshe kuuthibitishia umma kwamba nimechukua fomu ya urais,” alisema Shija.

Mgombea huyo ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sheria za Kodi na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ana Stashahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Fedha kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam na Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Uhasibu Arusha (IAA).

Pia Shija amehudhuria mafunzo mbalimbali ya uandishi wa habari na ameandikia magazeti mbalimbali hapa nchini kuanzia mwaka 1997.

Mgombea huyo aliwahi kuitumikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambaana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Kwa sasa ni Mhazini Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), akiwa pia amepata kuongoza klabu mbalimbali za mpira wa miguu kwa ngazi tofauti.

Mwaka 2008 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka wilayani Chato (CDFA), ambapo alisimamia usajili wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi ambao hata hivyo hakugombea. Pia Shija amepata kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Bukoba Veteran iliyopo mkoani Kagera.


That's an article BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF

Fine for article BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF This time, hopefully can benefit for you all. Well, see you in other article postings.

You are now reading the article BOSS TRA AJITOSA URAIS TFF With link address https://newstoday-ok.blogspot.com/2017/06/boss-tra-ajitosa-urais-tff.html

Subscribe to receive free email updates: